* Full name
* Date/year of birth + personal number in Norway (total of 11 numbers
including date/year of birth)
* Place of birth
* Nationality
* Previous nationality if any
* If not Norwegian citizen, pls. state immigration status and reference
No. with Norwegian Immigration Authorities
* Marital status
* Residential Address
* Employer (if any), and employer's address
* If not employed, how does the reference support him-/herself in
Norway?
In the invitation letter it has to be mentioned what kind of relationship the reference has to the applicant (if related, can this be proved?)
Introduction letter If this is a private visit and you are employed, then you should bring a letter from the employer confirming the employment, and that you will be given leave during the period for which you are applying for a visa.
Marriage certificate If you are married and travelling without your spouse, it is advisable that you bring and show your original marriage certificate
Confirmed return ticket to Tanzania. A print out will be sufficient to start with – PLS DO NOT PURCHASE YOUR TICKET BEFORE YOU ARE SURE THAT YOU WILL BE GRANTED A VISA!!
Travel Insurance must be valid for all Schengen countries – and each person must be insured for a minimum of 30.000 Euros
It takes a minimum of 5 working days to obtain a visa, so please allow enough time for this process.
Sometimes the Embassy forwards the application to the Directorate of Immigration in Oslo, Norway. When this is the case it can take up to 4 months to get a reply.
Visa fee, is currently at TAS 110.000 - has to be paid when handing in the application.
---------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Raia wa Tanzania wanaotaka kutembelea Norway wanahitaji kuomba viza. Mahitaji kwa ajili ya kuomba viza ya kwenda Norway inayoshughulikiwa na Ubalozi ni haya yafuatayo :
Fomu ya maombi – iliyojazwa kikamilifu na picha moja ya pasipoti. Picha hizo lazima ziwe za rangi, na zichukuliwe kwenye mandhari nyeupe kwa nyuma. USIBANE PICHA KWA PIN AU STAPLE. TUMIA PAPER CLIP!!
Pasipoti halali/hati ya usafiri. Pasipoti/hati ya usafiri lazima iwe halali kwa angalau miezi mitatu zaidi kuliko tarehe ya kurudi Tanzania na itambuliwe na sehemu zote kwa Makubaliano ya Schengen.
Fedha za kutosha. Ushahidi kwamba una uwezo wa kulipia ukaaji wako wa eneo la Schengen (taarifa ya pesa ya akaunti ya benki, hundi za usafiri, karatasi za mshahara)
au
Fomu ya dhamana iliyojazwa na mdhamini (mtu anayekualika). Fomu hii inaweza kupatikana katika kituo cha polisi cha nchini Norway na lazima ithibitishwe rasmi kabla ya kupelekwa – katika fomu halisi – kwenda kwa mwombaji au Ubalozini.
Barua ya mwaliko kutoka kwa mdhamini. Barua lazima iwe na taarifa zifuatazo:
* Jina kamili
* Tarehe/mwaka wa kuzaliwa + namba yako Norway (Jumla ya namba 11 ikiwa na tarehe/mwaka wa kuzaliwa)
* Mahali pa kuzaliwa
* Uraia
* Uraia wa mwanzo kama upo
* Kama wewe si raia wa Norway, tafadhali taja cheo chako na namba ya kumbukumbu ya Mamlaka ya Uhamiaji ya Norway
* Hati ya ndoa
* Anwani ya makazi
* Mwajiri (kama unaye), na anwani ya mwajiri
- Kama hukuajiriwa, mdhamini wako wa Norway anakusaidiaje?
Katika barua ya mwaliko inabidi itajwe aina ya uhusiano alionao mdhamini kwa mwombaji (kama wanahusiana, inaweza kuthibitishwa?)
Barua kutoka kwa mwajiri Kama ni safari ya binafsi na umeajiriwa, unatakiwa kuleta barua ya uthibitisho toka kwa mwajiri, vile vile athibitishe kuwa utapewa likizo kwa muda ulioomba viza
Cheti cha ndoa Kama umeoa/umeolewa na unasafiri bila mume/mke wako, unashauriwa kuleta cheti halisi (original) cha ndoa
Tiketi iliyothibitishwa ya kurudi Tanzania. Nakala ya kuchapisha inatosha kwa kuanzia – TAFADHALI USINUNUE TIKETI YAKO KABLA HUJAWA NA UHAKIKA KUWA UTAPEWA VIZA!!
Bima lazima iweze kutumika katika nchi zote za Schengen – na kila mtu lazima apate bima isiyopungua Euro 30.000
Kwa kawaida, inachukua siku za kazi zisizopungua 5 kupata viza, hivyo tafadhali toa nafasi ya kutosha kwa utaratibu huu kufanyika.
Wakati mwingine Ubalozi hulazimika kupeleka maombi kwa Ukurugenzi wa Uhamiaji mjini Oslo, Norway. Inapotokea hivi inaweza kuchukua mpaka miezi 4 kupata jibu.
Malipo ya Viza kwa sasa ni TAS 110.000. Lipa wakati wa kuleta maombi